- Shahidi aieleza mahakama wakati wa kutoa ushahidi wake katika kesi ya kutorosha nyara hazo
Moshi.
Afisa mstaafu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Miraji Msakamali
alishiki kusimamia utoroshwaji wa Twiga wanne kwenda Doha nchini Qatar
kwa niaba ya TRA.
Hayo
yalielezwa jana shahidi wa 26 ambaye ni Afisa Mfawidhi wa TRA Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA), Ngovore Ngovore wakati
akitoa ushahidi wake katika kesi hiyo.
Afisa
huyo alitoa ushahidi huo mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mkoa wa
Kilimanjaro, Simon Kobelo kwa kuongozwa na jopo la mawakili wa Serikali
wakiongozwa na Evetha Mushi.
Afisa
huyo alidai baada ya kupata taarifa hizo, aliiandikia Kampuni ya Equity
Aviation iliyoshughulikia mizigo hiyo na nakala kuzipa taasisi nyingine
zilizopaswa kuhusika.
Alizitaja
taasisi hizo kuwa ni Zoo Sanitary iliyopo chini ya Wizara ya Uvuvi na
mifugo, Kilimanjaro Aiport Development Company (Kadco) na Idara ya
Polisi uwanjani hapo.
Katika
barua hiyo, Zoo Sanitary walijibu kuwa usafirishwaji wa wanyama hao
haukufuata taratibu, lakini Kadco wao wakadai hawaoni tatizo kwa vile
taasisi zote zinazohusika zilishirikishwa.
“Kadco
walimtaja Miraji Msakamali kuwa alikuwepo usiku huo wakati wanyama hao
wakisafirishwa, lakini nilishangaa ilikuwaje mtumishi akarudi tena
kazini”alidai shahidi huyo.
Hata
hivyo, shahidi huyo alidai alipokutana na Msakamali ambaye sasa ni
marehemu na kumuuliza, alikanusha taarifa hizo na kueleza hakuingia
uwanjani kufanya kazi kama mtumishi wa TRA.
Shahidi
huyo alidai kuwa ingawa kwa utaratibu, TRA ilipaswa kuwa na kumbukumbu
za wanyama wote wanaoingia au kusafirishwa kwenda nje, katika
usafirishaji wa Twiga hawana nyaraka zozote.
Alidai
kuwa Novemba 24,2010, mshitakiwa wa tatu, Martin Kimati alifika ofisini
kwake akiwa na mtu mmoja mwenye asili ya Kihindi na kudai huyo Mhindi
anatarajia kusafirisha wanyama.
Shahidi
huyo alidai Kimath ambaye walikuwa wanafanya kazi wote Zoo Sanitary
ndiye aliyezungumza kwa niaba ya huyo Mhindi lakini hawakuwahi kurudi
tena ofisini kwake.
No comments:
Post a Comment