Pages

Thursday, July 3, 2014

KAMPUNI YA ORIFLAME YATAMBULISHA BIDHAA ZAKE KWENYE SOKO LA TANZANIA

Kampuni ya Vipozi vya aina mbalimbali vya urembo OriFlame wamefanya maonesho ya Bidhaa zao Tarehe 1.07.2014 katika ukumbi wa Zanzibar katika Hotel ya Hyatt Regency(The Kilimanjaro Hotel).
Kampuni hiyo yenye wigo mpana wa kibiashara ambayo ina matawi zaidi ya nchi 20 duniani na pia Katika Mabara manne ya Duniani wametambulisha bidhaa zao mpya kwenye soko la Tanzania ambazo ni marashi ya kike na kiume pamoja na vipodozi mbalimbali,
Juu Pichani ni  Maznat Yusuph Sinare kutoka saloon ya Maznat Bridal mtaalamu wa kuchanganya Vipodozi akimremba mwanadada Janeci Maluli ili kuonyesha aina tofauti za vipodozi vya Kampuni hiyo.
 Maza Yusuph Sinare  akimpaka wanja wa nyusi Mwanamitindo Janeci Maluli kwenye  sherehe za uzinduzi wa bidhaa mpya za kampuni ya ORIFLAME iliyofanyika kwenye ukumbi wa Zanzibar katika Hotel ya Hyatt Regency(The Kilimanjaro Hotel).
Mwanadada Janeci Maluli akiwa kwenye pozi baada ya kumaliza kurembwa kwa  kutumia Vipodozi vya kampuni ya ORIFLAME
Waandishi wa habari wakipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya ORIFLAME  Fortunata Nkya
Fredrick Njoka akizungumza jambo na mkuu wa masoko wa kampuni ya Vipodozi ya ORIFLAME, Harry Nyagi katika sherehe ya uzinduzi wa vipodozi vipya kwenye ukumbi wa Zanziba Hotel ya Hyatt Regency(The Kilimanjaro Hotel).
Mkurugenzi mkuu wa ORIFLAME katika upande wa Afrika ya Mashariki bwana Klas Kronaas (kushoto) akizungumza jambo na mkuu wa masoko wa kampuni ya Vipodozi ya ORIFLAME, Harry Nyagi (katikati) na kuliani mmoja wa wafanyakazi wa kampuni hiyo Bi. Fortunata Nkya

 Fortunata Nkya akizungumza na waandishi wa habari kwenye sherehe ya utambulisho wa bidhaa za ORIFLAME  katika soko la Tanzania
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya ORIFLAME katika upande wa Afrika ya Mashariki bwana Klas Kronaas akielezea namna bidhaa zao zinavyotengenezwa kwenye kwenye sherehe ya utambulisho wa bidhaa zao katika soko la Tanzania
Bi. Maznat Yusuph Sinare akieleza namna bidhaa na vipodozi mbalimbali vilivyokuwa na ubora wa kimataifa kwenye uzinduzi wa vipodozi vipya vya kampuni ya ORIFLAME kwenye ukumbi wa
 Maznat Yusuph Sinare akimpaka meck up mmoja wa warembo kwenye uzinduzi wa bidhaa mpya ya kampuni ya ORIFLAME
Mwanamitindo Neema Mbuya akipita jukwaani kuonesha moja ya Ripstick kwenye sherehe ya uzinduzi wa bidhaa mpya za kampuni ya ORIFLAME nchini Tanzania
 Mwanamitindo Annie Moses akiweka pozi la nguvu wakati akionesha Lipstick Ya kupaka mdomoni kwenye uzinduzi wa Bidhaa za kampuni ya ORIFLAME
Mwanamitindo Janeci Maluli alipita jukwaani akionesha moja  ya Ripstick kwenye sherehe ya uzinduzi wa bidhaa mpya ya kampuni ya ORIFLAME
Mkuu wa masoko wa kampuni ya Vipodozi ya ORIFLAME, Harry Nyagi akizungumza  jambo kwenye sherehe ya uzindizi wa bidhaa mpya za kampuni ya ORIFLAME
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya ORIFLAME katika upande wa Afrika ya Mashariki bwana Klas Kronaas akifanya uzinduzi rasmi kwa kufungua bango lililokuwa linaonesha bidhaa zao mpya
Mwonekano wa bidhaa zilizozinduliwa na kampuni ya ORIFLAME nchini Tanzania
Wageni walioalikwa kushuhudia uzinduzi huo wakijadiliana jambo kuhusiana na Bidhaa za kampuni ya ORIFLAME


Baadhi ya wadau waliofika kwenye uzinduzi huo wakifuatilia kwa makini maelekezo ya bidhaa za kampuni ya ORIFLAME

No comments:

Post a Comment