WATU watatu wanaotuhumiwa kuwa ni majambazi wameuwawa jijini Arusha walipokuwa katika harakati ya kwenda kupora mamilioni ya fedha zilizokuwa
zinapelekwa benki na kampuni ya Arusha Islamic Centre inayohusika na
utengenezaji na uuzaji wa vigae iliyopo eneo la Esso mjini
hapa.
Akizungumza
na waandishi wa habari ofisini kwake Jijini Arusha leo, Kamanda wa Polisi mkoani hapa,
Liberatus Sabas amesema kuwa,majambazi hao watatu waliuawa jana tarehe 3
eneo la TBL -Njiro wakiwa kwenye harakati za kwenda kupora
fedha hizo.
Alisema
kuwa, majambazi hao walikuwa mahali wanapanga njama majira ya saa 4;20
asubuhi wakisubiria kuteka gari lililokuwa limebeba fedha zilizokuwa
zinapelekwa benki zaidi ya milioni 100 huku wakiwa na gari aina ya
Toyota Corola yenye namba za usajili T 762 CWE.
Alisema
kuwa, raia wema walitoa taarifa kuhusiana na tukio hilo ndipo polisi
walifika eneo ambalo majambazi hao walikuwa wamejificha katika eneo la
unga ltd relini ambapo majambazi hao walishtuka na kuanza kuirishia gari
hiyo ya polisi risasi.
Kamanda
Sabas alisema kuwa,Askari wake walioona Majambazi hao wanawamiminia risasi kama mvua,ndipo na wao walipojibu mashambulizi na na kufanikiwa kuwawa kwa majambazi hao watatu na kufanikiwa kuchukua silaha yao aina ya shortgun yenye namba A 947514 M
aina ya Pumpaction ikiwa na risasi 3 .
Kamanda
alisema kuwa, bado majina ya majambazi hayo hayajafahamika ambapo
wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 25 hadi 30 na miili yao
imehifadhiwa katika hospitali ya mkoa ya mount Meru.
Aidha
Kamanda aliwashukuru wananchi kwa juhudi kubwa sana walizoonyesha na
ushirikiano hadi kukamatwa kwa majambazi hayo na kuwataka kuendelea
kuongeza juhudi hizo zaidi.
No comments:
Post a Comment