Pages

Friday, July 4, 2014

MWENYEKITI WA BODI YA MFUKO WA PENSHENI WA PPF, MH. RAMADHAN KIJJAH AVUTIWA NA UTENDAJI KAZI WA PPF KATIKA MAONYESHO YA 38 YA BIASHARA YA KIMATAIFA MAARUFU KAMA SABASABA‏

Mwenyekiti wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Mh Ramadhan Kijjah akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza kutembelea banda la PPF ili kujionea utendaji kazi wa Wafanyakazi wa PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba
Mmoja wa wateja waliotembelea banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam akijaza fomu ya kujiunga na Mfuko wa Pensheni wa PPF katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea kufanyika katika Viwanja vya Sabasaba.Anayemuelekeza Pembeni ni Afisa Huduma Kwa Wateja wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, BwMohamed Siaga
 Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF wakiwahudumia baadhi ya wateja waliofika katika banda la PPF kwenye maonyesho ya 38 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar Es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Katika Barabara ya Kilwa, Jijini Dar Es Salaam

 
Mwanasheria wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Nyambilila Ndoboka akitoa ufafanuzi kwa mteja aliyefika katika Banda la PPF kwaajili ya kupenda kufahamu hatua za kisheria zinazochukuliwa pindi pindi mwajili au mwanachama wa PPF anaposhindwa kuwasilisha Michango kwa Wakati kwenye Mfuko wa Pensheni wa PPF.
Afisa Mafao wa mfuko wa Pensheni wa PPF, Mercy Sammy akimuhudumia mmoja wa wateja waliofika katika banda la PPF kwenye maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam kwaajili ya Kujipatia huduma mbalimbali kutoka PPF.
 Afisa Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Anna Shayo akiwauhudumia wateja waliofika katika Banda la PPF kwaajili ya kupata maelekezo juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Mfuko huo wa PPF katika maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam.
 Afisa Mafao wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Hellen Mollel (kushoto) akitoa ufafanuzi wa maswali aliyoulizwa na mmoja wa wateja waliotembelea banda la PPF katika Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar Es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Barabara ya Kilwa Jijini Dar Es Salaam.Picha na Josephat Lukaza - Lukaza Blog

No comments:

Post a Comment