KIPA wa Newcastle, Tim Krul amekuwa shujaa wa Uholanzi baada ya kudaka mikwaju miwili ya penalti na kuipeleka timu yake nusu fainali wakati timu hiyo ilipokwaana na Costa Rica katika mechi ya robo rainali nchini Brazil usiku wa kuamkia leo.
Uholanzi wameshinda kwa penalti 4-3 na watakwaana na Argentina Julai 9 mwaka huu katika nusu fainali.
Kipa huyo aliingia sekunde chache kabla ya muda kabla ya muda wa nyongeza kumalizika akichukua nafasi ya kipa Jasper Cillessen.
No comments:
Post a Comment