Pages

Friday, July 18, 2014

MBUNGE WA CHALINZE RIDHIWANI KIKWETE AKABIDHI FEDHA,MIFUKO YA SARUJI KWA AJILI YA UJENZI WA VITUO VYA POLISI NA KOMPYUTA


1A
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akizungumza na uongozi wa polisi Mkoa wa Pwani na Wilaya ya Kipolisi ya Chalinze pamoja na wananchi waliojitokeza katika hafla ya makabidhiano ya vifaa mbalimbali kwa jeshi hilo zikiwemo kompyuta, mifuko ya Saruji pamoja na fedha vilivyotolewa na mbunge huyo, Kwa ajili ya kutatua matatizo mbalimbali yanayolikabili jeshi la polisi katika utekelezaji wa majukumu yake ya ulizni na usalama wa raia na mali zao. Pamoja na kukabidhi kompyuta hizo zitakazosaidia katika utunzaji wa kumbukumbu pia mbunge huyo ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya polisi vya Mbwewe na Kiwangwa ambavyo thamani inafikia zaidi ya shilingi milioni 11, Kushoto kwake ni Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei, hafla ya makabidhiano hayo imefanyika jana kwenye kituo kikuu cha polisi Chalinze.
1
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Kamanda ACP Ulrich Onesphory Matei zilizokabidhiwa na mbunge huyo kwa ajili ya kuboresha shughuli za jeshi hilo jimbo la Chalinze katikati ni Mkuu wa kituo cha polisi Chalinze Afande J. S. Magomi.

 
2
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kufungua ili kuonyesha kompyuta hizo huku viongozi wa jeshi hilo mkoani Pwani na jimbo la Chalinze wakishiriki shghuli hiyo.
3
Mbunge wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akimuonyesha moja ya kompyuta Kamanda wa polisi mkoa wa Pwani ACP Ulrich Onesphory Matei.

No comments:

Post a Comment