Timu ya Tanzania kwenye
Michezo ya Jumuiya ya Madola imewasili katika
uwanja wa
ndege wa Kimataifa Glasgow, Scotland jana usiku wa kuamkia leo kwa ndege
ya Shirika la ndege la Falme za Kiarabu (Emirates).
Jumla ya wanamichezo 42
waliwasili Uwanjani hapo na kupokelewa
na Afisa Ubalozi wa Tanzania London Bw. Amos Msanjila. Pamoja na
mapokezi na shamrashamra za wenyeji, baadhi ya Watanzania waishio Glasgow
walikuwepo Uwanjani hapo wakipeperusha bendera za Tanzania kuwahamasisha wanamichezo
hao.
Bw. Msanjila
akimlaki Nahodha wa Timu hiyo Selemani Kidunda. Katikati ni Kiongozi wa Msafara Bw. Muharami Mchume
Bw. Msanjila
akimkabidhi bendera ya Tanzania Nahodha wa Timu hiyo Selemani Kidunda.
Baadhi ya Watanzania na marafiki zao waishio Glasgow walikuwepo Uwanjani hapo wakipeperusha bendera za Tanzania
kuwahamasisha wanamichezo hao. Michezo ya Jumuiya ya
Madola inayotarajiwa kufunguliwa rasmi Jumatano (23 Julai 2014) na Malkia
Elizabeth wa Pili itajumuisha nchi na Himaya 70. Michezo hiyo itafungwa tarehe
3 Agosti 2014.
No comments:
Post a Comment