Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Friday, July 4, 2014

MWANA WA MFALME WA JAPAN PRINCE AKISHINO AWASILI ZANZIBAR NA KUONANA NA RAIS DKT SHEIN


Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino alieambatana na Mkewe Princess Akishino wakiteremka kutoka kwenye ndege katika Uwanja wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume kuanza ziara ya siku moja hapa Zanzibar.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Ikulu na Utawala Bora Mwinyihaji Makame akimlaki Mwana  Mfalme wa Japan Prince Akishino alieambatana na makewe Princess Akishino katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume Chukwani Zanzibar.


Mtoto akimvisha shada la Mauwa Mwana Mfalme wa Japan Akishino alipowasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aamani Karume Chukwani Zanzibar.



Mwana  Mfalme wa Japan Akishino akisalimiana na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Maalim Abdalla Mwinyi Khamis alipowasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Amani Abeid Karume Chukwani Zanzibar.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Muhamed Shein akimlaki Mwana Mfalme wa Japan Prince Akishino alipofika Ikulu Mjini Zanzibar kwa mazungumzo.
(Picha na Makame Mshenga wa Maelezo Zanzibar).

No comments:

Post a Comment