Nahodha wa timu ya taifa ya Ujerumani Philipp Lahm amestaafu
kucheza soka la kimataifa, baada ya kukiongoza kikosi chake na kushinda Kombe
la Dunia nchini Brazil.
Beki huyo wa Bayern Munich, ambaye pia anaweza kucheza kama
kiungo, ameichezea Ujerumani mara 113.
Lahm, 30, ataendelea kucheza Bayern Munich, ambapo amesaini
mkataba hadi mwaka
2018. Habari za kustaafu kwake kuichezea timu ya taifa
zimethibitishwa na chama cha soka cha Ujerumani DFB.
Lahm alianza kuichezea Ujerumani Februari 2004 walipoichapa
Croatia 2-1, na amestaafu kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya Argentina katika fainali
ya Kombe la Dunia.
No comments:
Post a Comment