Pages

Saturday, July 5, 2014

NIGERIA IMEWAKAMATA BOKO HARAM WANAWAKE.


Jeshi nchini Nigeria linasema limewakamata wanawake watatu ambao walikua wanawaandikisha wafuasi wanawake kwa kundi la siasa kali za Kiislamu la Boko Haram.

Inadaiwa wanawake hao waliwalenga wajane na wasichana wadogo wakiwaahidi kuwachumbia kwa wafuasi wa Boko Haram.

Mwaandishi wa BBC Will Ross akiwa Abuja anasema inaelekea Boko Haram inajaribu kuwashawishi wanawake washiriki vilivyo katika mapambano yao.

Hafsat Usman Bako ni mmoja wa wale waliokamatwa

Mwezi uliopita mshambuliaji mwanamke wa kujitoa mhanga alifariki alipojaribu kuishambulia kambo ya kijeshi katika jimbo la Gombe - tukio la kwanza aina hiyo nchini Nigeria.

Bomu hilo lililipuka alipokua akipekuliwa katika kituo cha usalama . Mwanajeshi mmoja pia aliuwawa.




Wanawake pia ni miongoni mwa wale waliokamatwa na kuzuiliwa katika miji ya Maiduguri kaskazini mwa Nigeria, eneo ambalo Boko Haram wanaungwa mkono kiasi .

Jeshi la Nigeria limesema wanawake watatu iliowakamata walikuwa ni wa tawi la upelelezi.

Ilisemekana mmoja wao alikua ni mjane wa mpiganaji wa Boko Haram.

Kundi hilo la wanaharakati wa Kiislamu bado linawashikilia zaidi ya wasichana wa shule 200 iliowakamata mnamo mwezi wa Aprili katika mji wa Chibok katika jimbo la Borno .

Boko Haram inadai wapiganaji wake na jamaa zao waachiliwe kwa kubadilishana na wasichana.Serikali imelikataa dai hilo

No comments:

Post a Comment