Jeshi nchini Nigeria linasema limewakamata wanawake watatu
ambao walikua wanawaandikisha wafuasi wanawake kwa kundi la siasa kali za
Kiislamu la Boko Haram.
Inadaiwa wanawake hao waliwalenga wajane na wasichana wadogo
wakiwaahidi kuwachumbia kwa wafuasi wa Boko Haram.
Mwaandishi wa BBC Will Ross akiwa Abuja anasema inaelekea
Boko Haram inajaribu kuwashawishi wanawake washiriki vilivyo katika mapambano
yao.
Hafsat Usman Bako ni mmoja wa wale waliokamatwa
|
Mwezi uliopita mshambuliaji mwanamke wa kujitoa mhanga
alifariki alipojaribu kuishambulia kambo ya kijeshi katika jimbo la Gombe -
tukio la kwanza aina hiyo nchini Nigeria.
Bomu hilo lililipuka alipokua akipekuliwa katika kituo cha
usalama . Mwanajeshi mmoja pia aliuwawa.
Wanawake pia ni miongoni mwa wale waliokamatwa na kuzuiliwa
katika miji ya Maiduguri kaskazini mwa Nigeria, eneo ambalo Boko Haram
wanaungwa mkono kiasi .
Jeshi la Nigeria limesema wanawake watatu iliowakamata
walikuwa ni wa tawi la upelelezi.
Ilisemekana mmoja wao alikua ni mjane wa mpiganaji wa Boko
Haram.
Kundi hilo la wanaharakati wa Kiislamu bado linawashikilia
zaidi ya wasichana wa shule 200 iliowakamata mnamo mwezi wa Aprili katika mji
wa Chibok katika jimbo la Borno .
Boko Haram inadai wapiganaji wake na jamaa zao waachiliwe
kwa kubadilishana na wasichana.Serikali imelikataa dai hilo
No comments:
Post a Comment