Washiriki wa Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) wakiwa jukwaani wakati wakiigiza moja ya Igizo walilopewa na Mwalimu wao Dk Mona Mwakalinga katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa siku ya Jumanne ya Wiki inayomalizika leo.Igizo hilo ni la kwanza kwaajili ya mchujo kwa washiriki
Vijana wakiendelea na Kazi Jukwaani
Vijana wakiwajibika katika jukwaa kwaajili ya kuwania tiketi ya kuzisaka Milioni 50 za kitanzania katika fainali itakayofanyika mwisho wa mwezi wa nane.
Josephat Lukaza - Proin Promotions Limited - Dar Es Salaam.
Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) limeingia hatua nyingine ambapo sasa washiriki wa fainali ya Shindano hilo kuanza kupigiwa kura na watazamaji. Washiriki hao 20 kutoka kanda sita za Tanzania wanaendelea na kambi huku wakipewa mafunzo juu ya sanaa ya uigizaji na uandikaji wa muswada (script) kutoka Kwa Mhadhiri wa Sanaa kutoka Chuo Kikuu Cha Dar Es Salaam, Dk Mona Mwakalinga.
Washiriki hao 20 sasa watapigiwa kura na watazamaji kutoka na kuonyesha uwezo wao wa kuigiza na kuwavutia watazamaji kwa vipaji vyao. Kipindi cha Kwanza cha Mchujo kimeonyeshwa hapo jana Kupitia kituo cha Runinga cha ITV ambapo sasa watazamaji wameweza kujionea uwezo wa kila Mshiriki katika Shindano hilo.
Vipindi vya TMT vitaendelea kurushwa kupitia ITV kila Jumamosi saa NNE USIKU na kurudiwa Jumapili Saa KUMI JIONI na JUMATANO SAA TANO USIKU, usikose kutazama ni mshiriki yupi mwenye uwezo na aliyekuvutia ili uweze kumpigia kumpigia kura
Jinsi ya Kumpigia Kura Mshiriki umpendae unaenda upande wa Meseji kwenye Simu yako na Kuandika "TMT" ikifuatiwa na Namba ya Mshiriki halafu unatuma kwenda 15678. Mfano: TMT00 halafu unatuma kwenda 15678. Vigezo na masharti kuzingatiwa.
Fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents litafanyika Mwisho wa Mwezi wa Nane ambapo mshindi mmoja atajinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
No comments:
Post a Comment