Pages

Saturday, July 26, 2014

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOANI DODOMA KUHUSU MUIMBAJI WA INJILI BAHATI BUKUKU ALIVYOPATA AJALI MKOANI DODOMA AKIELEKEA KAHAMA KWENYE TAMASHA.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dodoma David Misime - SACP

Na: Sylvester Onesmo wa Jeshi la Polisi Dodoma
Gari lenye namba IT 7945 aina ya Toyota Nadia ikiendeshwa na EDSON S/O MWAKABUNGU, Mnyakyusa, Miaka 31 mkazi wa Tabata – Dar es Salaam liliacha njia na kugonga gema na kusababisha majeruhi kwa watu watatu baada ya kugongwa na gari lingine linalosadikiwa kuwa ni Fuso.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME – SACP amesema ajali hiyo imetokea tarehe 


26.07.2014 majira ya saa 03:00 alfajiri katika barabara kuu ya Morogoro – Dodoma eneo la Ranch ya NARCO Wilaya ya Kongwa.
Kamanda MISIME amewataja waliojeruhiwa katika ajali hiyo kuwa ni EDSON s/o MWAKABUNGU ambaye analalamika maumivu sehemu za vidole vya miguu yote, BAHATI D/O BUKUKU, Miaka 40, Mnyakyusa, Msanii wa nyimbo za Injili na mkazi wa Tabata – Dar es Salaam ambaye analalamika maumivu sehemu mbalimbali za mwili wake na FRANK S/O CHRISTOPHER, Muha, Miaka 20, Msanii wa muziki wa Injili mkazi wa Tabata Dar es Salaam yeye ana michubuko usoni na mkono wa kulia. Wote wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kongwa kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuri.
Aidha Kamanda MISIME ameongeza kwa kusema kuwa watu walikuwa wanatokea Dar es Salaam ambapo dereva alikuwa anelekea DRC – Kongo, BAHATI d/o BUKUKU na FRANK s/o CHRISTOPHER walikuwa wanakwenda Kahama kwenye tamasha la Injili.
Uchunguzi wa ajali hii unaendelea ikiwa ni pamoja na kutafuta gari lililowagonga.

No comments:

Post a Comment