Mtuhumiwa wa Kesi ya jinai, Yasinta Rwechengura mkazi wa Boko-Magengeni,
Dar anayetuhumiwa kwa kumjeruhi mfanyakazi wake wa ndani aitwaye Melina
Mathayo (15) kwa kumpiga na nyaya za Kompyuta na kwanja la kuzolea
majani maarufu kama leki na kumsababishia majeraha makubwa kichwani na
sehemu nyingine za mwili ameendelea kusota rumande.
Mtuhumiwa wa kesi ya kumtesa hausigeli wake, Yasinta Rwechengura baada ya kushuka kutoka kwenye gari la magereza akielekea kizimbani chizi ya ulinzi mkali wa askari magereza.
Ndugu wa Yasinta wakiwa nje ya jengo la Mahakama ya Kinondoni kabla ya mtuhumiwa huyo kupandishwa kizimbani.
Tukio hilo la kikatili lilitokea mapema Juni 11, mwaka huu majira ya saa
3 usiku maeneo ya Boko, nje kidogo ya Dar baada ya mwenye nyumba huyo
kufanya kitendo hicho kwa madai ya kuwa mfanyakazi wake huyo alikuwa
kiburi kila alipomtuma kazi za ndani.
Mtuhumiwa Yasinta akiwa chini ya Ulinzi baada ya kesi yake kuahirishwa mpaka Julai 11 mwaka huu itakaposomwa baada ya kupangiwa hakimu mpya.
Akisoma
shitaka hilo, Wakili wa Serikali, Credo Lugaju mbele ya Hakimu Mkazi
Boniphace Lihamwike alisema kuwa kesi hiyo imeahirishwa kutokana na
hudhuru mbalimbali uliojitokeza kwa Hakimu wa awali aliyepangiwa kesi
hiyo.
Kesi hiyo itasikilizwa tena Julai 11 mwaka huu baada ya kupangiwa hakimu mpya na mtuhumiwa kurudishwa rumande.
CHANZO: GPL
No comments:
Post a Comment