Shao Zongqi akiwa mahakamani
Waswahili husema wivu ni kidonda ukiushiriki utakonda .kauli
hii inakuja baada ya mwanamume mmoja kuua watu 6 baada ya mkewe kujihusisha na
wanaume hao kingono,kutokana na tukio hilo mwanamume huyo amehukumiwa adhabu ya
kifo nchini China.
Shao Zongqi, mwenye umri wa miaka 38 alikutwa na hatia baada
ya kutekeleza mauaji hayo mwezi January mwaka huu, alipoua katika mji wa
Yunnan.
Kwa muujibu wa mahakama,Shao alipanga kulipiza kisasi baada
ya kugundua kua mkewe alikua na mahusiano na wanaume wawili tofauti,shirika la
habari la Xinhua limeeleza hayo.
Wakati wa sherehe za mwaka mpya wa kichina,Shao alijeruhi
wanaume tisa, na kumuua mmoja pamoja na familia yake na wanaume wengine wawili
wa jirani,wakati mwanamume mmoja akiwa na mkewe na mtoto wao wa kiume
walinusurika katika tukio hilo.
Wakati hukumu hiyo ikitolewa siku ya jumatatu, iliamuriwa
Shao alipe kiasi cha yuani 604,000/- sawa na dola za kimarekani 98,000/- kwa
familia walio hai ambao waliondokewa na jamaa zao kutokana na shambulio
hilo.Pamoja na kulipa faini hiyo Shao ameapa kukata rufaa kutokana na hukumu
hiyo ya kifo inayomkabili.
No comments:
Post a Comment