Madaktari nchini Uingereza wameumba masikio kutokana na
ubavu wa kijana aliyezaliwa bila ya viungo hivyo muhimu.
Kijana huyo wa miaka tisa Kieran Sorkin alizaliwa bila
masikio na madaktari wamekuwa wakifanya majaribio ya mbinu mpya ya matibabu
katika hospitali ya Great Ormond Street iliyoko jijini London..
Taarifa zinazohusiana
afya
Takwimu nchini Uingereza zinaonesha kuwa takriban watoto 100
huzaliwa bila kiungo hicho muhimu nchini Uingereza .
Madaktari wanaita ugonjwa huo microtia.
Kieran aliyezaliwa kama kiziwi hakuwa na masikio alipozaliwa
badala yake alizaliwa na shimo mbili na ndewe tu badala ya masikio.
Tayari kieran anasikia baada ya upasuaji wa awli ambao
ulimsaidia kupandikiza kifaa kinachomsaidia kupaza sauti ndani ya masikio yake.
"Ningependa watu wakome kuniuliza kwanini unakaa
tofauti hivi ", alisema Kieran akiwa katika mtaa wa Hertfordshire.
"nimefurahishwa sana kufanana na marafiki wangu ''.
"Hata mimi ninafurahi kuwa sasa nitaweza kuvaa miwani
na vifaa vya kusikizia muziki."
Madaktari waunda masikio toka ubavuni mwa kijana mwenye
miaka 9
Mamake Kieran ,Louise Sorkin alisema kuwa kijana huyo ni
mchangamfu sana na alikuwa anasubiri kwa hamu kufanyiwa upasuaji wa kupandikiza
masikio hayo.
"Sikuwa nafurahiwa watoto wenzake wakimkejeli kutokana
na maumbile yake."
Asubuhi ya siku ya upasuaji huo Neil Bulstrode aliumba
masikio hayo na akapandikiza akitumia teknolojia ya kisasa ya kushona masikio
hayo chini ya ngozi ya kichwa chake .
Wanasayansi hao wanasema kuwa walitumia mbinu mpya ya kukuza
viungo hivyo.
Kieran alifurahishwa sana alipooeshwa masikio yake mapya
siku tatu baada ya operesheni hiyo.
No comments:
Post a Comment