Julio Cesar sasa atacheza Ligi ya Mabingwa baada ya kusaini
Benfica ya Ureno
KLABU ya Benfica imekamilisha usajili wa kipa wa kimataifa
wa Brazil, Julio Cesar kwa mkataba wa miaka miwili kutoka QPR.
Mlinda mlango huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 34 alijiunga
na klabu hiyo ya London mwaka 2012, lakini akacheza mechi 24 kabla ya kwenda
kwa mkopo Toronto.
Robert Green amechukua nafasi yake kama kipa wa kwanza wa
klabu hiyo na Benfica imeamua kumchukua kipa huyo aliidakia Brazil iliyofanya
vibaya Kombe la Dunia mwaka huu.
No comments:
Post a Comment