USAJILI wa kiungo Arturo Vidal kutoka Juventus kwenda
Manchester United umepata ganzi kufuatia mashaka ya kutokuwa fiti kwa nyota
huyo wa Chile, hii ni kwa mujibu wa kocha wake wa timu ya
taifa.Kocha wa Chile
Jorge Sampaoli ameliambia gazeti la El Mercurio la nchini humo kuwa bosi wa
United, Louis van Gaal anahofia kutumia pauni milioni 47 kwa Arturo Vidal
ambaye aliandamwa na maumivu ya goti.
Vidal amekuwa akiwindwa na United na kwa muda mrefu ambapo
katika muda wote wa dirisha la usajili la kiangazi, usajili wake wa kwenda Old
Trafford umekuwa ukionekana uko jirani.
“Najua tatizo kubwa la usajili wake wa pauni milioni 47
kwenda Manchester United ni Van Gaal kuwa na mashaka na maendeleo ya goti la
Vidal,” alisema kocha Jorge Sampaoli.
Kocha huyo wa Chile raia wa Argentina, alisema ana uhakika
Vidal alionyesha kiwango cha asilimia 30 au 40 tu katika michuano ya kombe la
dunia kulinganisha na ubora wake uliozoeleka Juventus.
No comments:
Post a Comment