Pages

Wednesday, August 6, 2014

MADEREVA WA PIKIPIKI WAVAMIA KITUO CHA POLISI NA KUJERUHI ASKARI NA KUMTOROSHA MTUHUMIWA

Madereva wa pikipiki wamevamia kituo cha polisi cha  kinone mvuha wilaya ya Morogoro kwa kupiga mawe na kumjeruhi askari mmoja na kisha kumtorosha mtuhumiwa aliekuwa anashikiliwa kwa makosa ya kubebe abiria watatu katika pikipiki moja.

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul  akizungumza na vyombo vya habari  amesema 


madereva hao walikua wakishinikiza mwenzao kuachiliwa huru ambapo  kabla ya tukio madereva wa pikipiki walifanya mgomo kisha kuandamana  ambapo  alivamia kituo cha polisi na kupiga mawe na kumjeruhi askari mmoja na kufanikiwa kumtorosha mtuhumiwa  ambapo jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watu 18 wanaosadikiwa kuhusika na tukio hilo na watafikishwa mahakamani.

No comments:

Post a Comment