Upande wa mashitaka katika kesi ya mauaji inayomkabili
mwanaridha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, imeanza kutoa kauli yake ya
mwisho kuhusiana na kesi hiyo.
Hii ni kabla ya mahakama kutoa umauzi wake wa
mwisho kuhusu
hatma ya mwanariadha huyo.
Bwana Pistorius anatuhumiwa kwa mauaji ya mpanzi wake, Reeva
Steenkamp, nyumbani kwake mjini Pretoria mwaka jana.
Wakili wa upande wa mashitaka Gerrie Nel amesema sio ukweli
kuwa Pistorius alimpiga risasi mpenzi wake kimakosa akidhani kwamba alikuwa
jambazi.
Mauaji hayo yalitokea tarehe 14 mwezi Februari mwaka jana
. Kiongozi wa mashitaka Gerrie Nel
Wakili wa Pistorius pia anatarajiwa kutoa kauli yake ya
mwisho kuhusiana na kesi hiyo.
Kesi hiyo iliahirishwa mwezi jana kablahatua hii ya pande
zote kutoa kauli zao za mwisho kabla ya kesi kuamuliwa kufika.
Bwana Pistorius alisema alimpiga risasi Reeva kutokana na
uoga kwani alidhani alikuwa mwizi aliyekuwa amevamia nyumba yake.
Hata hivyo wakili wa upinzani ameambia mahakama haipaswi
kuwa a ugumu wowote katika kukataa ushahidi wa Pistorius kwa sababu hauna
msingi na kwamba ni uongo.
Pia amesema Pistorius amejidai kuwa mwathiriwa kwa njia moja
au nyingine kutokana na ulemavu wake.
Babake Pistorois ambaye hajakuwa maishan mwake kwa miaka
mingi alikuwa mahakamani kwa mara ya kwanza tangu kesi hiyo kuanza kusikilizwa.
Babake marehemu Reeva pia alifika mahakamani kwa mara ya kwanza.
No comments:
Post a Comment