Urusi imetangaza marufuku ya vyakula kutoka kwa muungano wa
Ulaya, Marekani na nchi zingine kadha za magharibi ambazo zilikuwa zimetangaza
vikwazo dhidi ya Urusi kutokana na sera zake nchini Ukraine.
Waziri mkuu nchini Urusi Dmitry Medvedev aliuambia
mkutano
wa serikali kuwa Urusi haitaruhusu tena uingizwaji wa Nyama, Samaki, Matunda na
bidhaa zingine kutoka mwa jumuiya ya Ulaya, Marekani, Australia, Canada na
Norway.
Medvedev amesema kuwa vikwazo hivyo vitadumu kwa kipindi cha
mwaka mmoja.
Amesema kuwa Urusi inatathmini kupiga marufu mashirika ya
ndege ya nchi za magharibi yanayotumia anga ya Urusi kuingia barani Asia.
Wadadisi wanasema kuwa Urusi inategemea zaidi chakula kutoka
nje asilimia kubwa ikiwa ni kutoka kwa nchi za magharibi.
No comments:
Post a Comment