Kaonja ladha ya Camp Nou: Suarez aliingia akitokea benchi katika dakika ya 75 na kucheza mechi yake ya kwanza Barcelona.
Bado ana miezi miwili zaidi ili kuanza rasmi kucheza, lakini Luis Suarez tayari ameonja kelele za Camp Nou zikishangilia jina lake.
Hatimaye mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool ametambulishwa kwa mashabiki wa Barcelona jumatatu usiku kabla ya Barca kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya FC Leon, wiki tano baada ya kujiunga na klabu, na siku nne baada ya kifungo cha FIFA cha kutojihusisha na shughuli zote za michezo kuondolewa.
Saa moja kabla ya kuanza kwa mechi ya mwisho ya maandalizi ya msimu kwa Barcelona, uwanja haukufurika sana, lakini kulikuwa na shangwe za kutosha na jina lake liliimbwa akiwa amevalia jezi namba 9.
Namba yako hii baba!: Luis Suarez alitokea benchi akivalia jezi namba 9
Akaanza mambo: Mshambuliaji wa zamani wa Liverpool hakucheza sana mpira katika mechi yake ya utambulisho
Lionel Messi akichuana na mabeki wa Leon FC
Lionel Messi alifungua karamu ya mabao ya Barcelona akifunga bao la kuongoza katika dakika ya tatu ya mchezo
Hakuna mashaka: Lionel Messi akishangilia bao lake na Neymar baada ya Brazil huyo kutoa pasi ya goli hilo.
Kijana kutoka Brazil: Neymar alionekana kuimarika baada ya kuifungia bao la pili Barcelona katika kipindi cha kwanza.
No comments:
Post a Comment