Madereva wa pikipiki wamevamia kituo cha polisi cha kinone mvuha wilaya ya Morogoro kwa kupiga
mawe na kumjeruhi askari mmoja na kisha kumtorosha mtuhumiwa aliekuwa
anashikiliwa kwa makosa ya kubebe abiria watatu katika pikipiki moja.
Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro Leonard Paul akizungumza na vyombo vya habari amesema
madereva hao walikua wakishinikiza
mwenzao kuachiliwa huru ambapo kabla ya
tukio madereva wa pikipiki walifanya mgomo kisha kuandamana ambapo
alivamia kituo cha polisi na kupiga mawe na kumjeruhi askari mmoja na
kufanikiwa kumtorosha mtuhumiwa ambapo
jeshi la polisi limefanikiwa kuwakamata watu 18 wanaosadikiwa kuhusika na tukio
hilo na watafikishwa mahakamani.
No comments:
Post a Comment