Pages
▼
Saturday, August 30, 2014
MAJAMBAZI YAFANYA KUFURU SIMIYU, YAPORA SH20 MIL KISHA KUMKABA MWALIMU WA KIKE
Watu wanaosadikiwa kuwa majambazi wanadaiwa kumvamia mwalimu mmoja, wampora zaidi ya Sh. milioni 20 na kumbaka mwalimu mwingine na kutokomea.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Nassa Ginery, wilayani Busega mkoani Simiyu.
Polisi mkoa wa Simiyu imethibitisha kutokea kwa tukio hilo usiku wa kuamkia juzi.
Akisimulia tukio, mwalimu aliyepatwa na mkasa huo, Samwel Mbochi alisema watu hao waliruka ukuta wa nyumba yake na kumvamia na kuanza kumshambulia mwilini na kudai awape pesa.
Alisema kuwa pesa hizo alikuwa ameziandaa kwa ajili ya kununua bidhaa kesho yake kwa kuwa amekuwa akijishughulisha na biashara ya duka.
Alisema baada ya kuchukua pesa hizo, watu hao walimvamia mpangaji wake katika chumba kingine ambaye pia ni mwalimu na kumbaka kwa zamu kisha kutokomea kusikojulikana.
Afisa upelelezi wa makosa ya jinai mkoani Simiyu, Evance Mwijage jana alithibitisha kuwapo kwa tukio hilo.
Mwijage alisema atawataja watu waliohusika kwenye tukio hilo mara baada ya kupata taarifa rasmi kutoka polisi. CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment