Pages

Wednesday, August 20, 2014

MANENO YA DIAMOND KWA WEMA SEPETU YAMCHOMA AUNTY EZEKIEL



Star wa filamu nchini Aunty Ezekiel anadaiwa kuchomwa vilivyo na maneno ya Diamond kwa Wema Sepetu yanayodaiwa kumgusa yeye pia moja kwa moja kama rafiki wa Wema...
Diamond juzi alisema  kuwa Wema anapenda sana starehe na mashoga wapenda kujirusha badala ya kufanya kazi ili kujiletea maendeleo kwa kutumia fursa aliyonayo sasa.Kwa mujibu wa chanzo kilicho karibu na Aunty kikizungumza  jana kwa sharti la kutotajwa jina kilisema kuwa baada ya Aunty kuona alichoandika Diamond aliachia msonyo wa kufa mtu kuonyesha hakupendezwa hata kidogo huku akibaki kuumia.



"Aunty alipoona alichoandika Diamond alichia msonyo huoo! unajua maneno ya Diamond yamejaa ukweli mtupu, yalikuwa kama mkuki kwa Aunty, Aunty ni mtu wa starehe sana si umeona hata ndoa yake haina uhai, ukweli unauma, yeye na Wema wanapaswa kujiangalia upya Diamond amempa Wema ushauri mzuri sababu anampenda"

Chanzo hicho kilisema kuwa Aunty anataka kukata ukaribu wake na Wema ili kuepusha maneno kwasababu ameshazoea kuishi kwa kujirusha.

"Urafiki wa Wema  na Aunty muda si mrefu utakuwa kama ule wa Kajala, Aunty anataka kumuacha Wema na bwana'ke yeye achukue hamsini zake"kilisenma chanzo hicho

Hata hivyo Aunty alipotafutwa  ili kutoa ufafanuzi hakupatikana .

No comments:

Post a Comment