STAA wa filamu za Kibongo, Deogratius Shija ameugua ghafla
na kulazwa katika hospitali moja jijini Johannesburg, Afrika Kusini alipokwenda
kwa mapumziko mafupi.
Akiwasiliana na mwandishi wetu kupitia
mtandao mmoja wa
kijamii, rafiki wa karibu wa Shija aliyeomba hifadhi ya jina lake alithibitisha
kuhusu kuugua kwa msanii huyo.
Ni kweli Shija amelazwa hapa Kwazulu Natal, aligua ghafla
kutokana na mbadilishano wa hali ya hewa.
Hapa Sauzi kipindi hiki kuna baridi kali sana. Kwa huko
Bongo, unaweza kufananisha na Mufindi, lakini hali yake siyo mbaya sana,
anaendelea vizuri
alisema rafiki huyo ambaye ndiye mwenyeji wa Shija.
Siku ya pili, mwandishi wetu alifanikiwa kuwasiliana na
Shija kupitia mtandao mwingine wa kijamii ambapo alisema:
Ni kweli kaka nilipata dhoruba la afya kidogo, lakini
nashukuru sasa nipo poa na nimeshatoka hospitalini.
No comments:
Post a Comment