Mwili wa Fredrick Mgaya (60) ukiwa unaning’inia katika mti
aliojinyongea , Tunaomba radhi kwa picha hii.
Na Mwandishi wetu Peramiho
Songea Mwanaume mmoja
Fredrick Mgaya (60), mkazi wa Peramiho, Songea mkoani Ruvuma amejinyonga usiku
wa kuamkia leo katika maeneo yaliyo karibu na viwanja vya michezo vya Abasia
kijijini Peramiho.Mwanaume huyo aliyekuwa
akifanya kazi kitengo cha maabara
katika Hospitali ya Peramiho na kustaafu mnamo mwezi aprili mwaka huu amekutwa
amejinyonga majira ya asubuhi ya leo. Marehemu Fredrick Mgaya amekutwa na
ujumbe katika mfuko wa shati lake, ulioelezea chanzo kilichopelekea yeye
kujitoa uhai. Afande Allen Urio ambaye alikuwa mmoja wa mashuhuda wa
kwanza,anasema “ Nilikuwa natoka lindo asubuhi ndipo nikakuta kundi la
wanafunzi wa shule ya msingi wakiwa njiani, nikawauliza kwanini wamesimama
badala ya kwenda shule muda ule, ndipo waliponiambia kuna mtu ananing’inia
kwenye mti pale.
Nilipofika kwenye mti huu ndipo nilipomkuta mzee wetu
Fredrick Mgaya akiwa ameshapoteza maisha.
Ni tukio la kusikitisha sana kwani ni mzee wetu katika jamii
ambaye tulikuwa tunaishi naye vizuri. Mbali na migogoro yake na mkewe lakini
uamuzi aliouchukuwa unasikitisha na si mzuri kabisa.
Kama mlinda amani katika jamii napenda kuwaasa wananchi
wajaribu kutafuta suluhu ya matatizo kwa namna nyingine na sio kwa kujitoa
uhai”
Akiongea Hakimu wa
mahakama ya mwanzo kijijini Peramiho bi Maria Sambo amesema, ameshaletewa na
kusuluhisha migogoro ya ndoa hiyo ya marehemu mara mbili na hadi sasa kuna kesi
inayoendelea katika mahakama ya Hakimu mkazi, lakini kwa hali ya kawaida hakudhani kwamba marehemu
Fredrick Mgaya angefikia hatua hiyo ya kujitoa uhai.
Nao mashuhuda wa tukio hilo wakiongea kwa masikitiko, wengi
wamelaani uamuzi uliofikiwa na mzee Mgaya kwani ni dhahiri alikuwa ni mtu wa
watu na pia alikuwa ni tegemeo la familia yake ambayo amewaacha ghafla.
Uamuzi ambao umesababisha maumivu kwa wanajamii hususan
ndugu, jamaa pamoja na marafiki wengi waliokuwa wakimpenda na kushirikiana naye
kwa mambo mengi ya kimaisha.
Mwenyekiti wa kijiji cha Peramiho A Bwana Joseph Ngonyani
ameonesha masikitiko yake ya dhati kwa kuondokewa na moja ya wazee aliokuwa
akiwategemea kwa ushauri katika kijiji chake.
“Tukio hili linagusa
sana unajua, kwasababu linahusu mtu wa karibu sana na ambaye tunashinda nae
siku zote bila kujua nini kinamsibu na nini anakipanga katika akili yake”.
Ndoa nyingi sana zinasumbuliwa na migogoro ya hapa na pale,
hivyo ni vizuri watu wa ustawi wa jamii na asasi zinazohusiana na jamii
kujaribu kutoa mafunzo na maelekezo ya jinsi ya kutatua migogoro hiyo ili
kuepusha adha kama hii isijitokeze tena ndani ya jamii yetu.
Alisema mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo bwana Ignasi
Kapinga.
Winfried Thadei
Mgaya, mdogo wa marehemu anasema, amepokea tukio hilo kwa mshtuko na kwa
majonzi sana. Anapata uchungu sana juu ya msiba wa kaka yake kwani marehemu
ameacha watoto wanne ambao bado ni tegemezi pamoja na mjane. Pia amesema
mazishi yatafanyika tarehe 7 jumamosi
kijijini kwao Madaba, Songea mkoani Ruvuma.Habari kwa hisani ya
Demashonews
No comments:
Post a Comment