Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na Kondakta wa Gali
lililopata ajali mara baada ya Kumnasua kwenye roli hilo.Kijana anaonekana
kuuguria maumivu makali kwenye Mkono.
|
Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia sehemu aliyokuwa amebanwa
Kondakta wakati Roli hilo likianguka na baadae kuinuka kutokana na kugonga
Ukuta pembezoni mwa Barabara ya Iringa-Morogoro.
Mh:Mwigulu Nchemba akitoka huduma ya Kwanza kwa Majeruhi wa
ajali hiyo.
|
Huyu ni Dreva akijaribu kuwasha Gari hilo.
|
Mh:Mwigulu Nchemba akiendelea kutoa huduma ya kwanza kwa
Majeruhi kabla ya kumkimbiza kwenda
hospitali ya WIlaya ya Mikumi.
Naibu waziri wa Fedha na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Tanzania Bara Mh:Mwigulu Nchemba jana alifanya jambo
kubwa na lakibinadamu kwa kuamua kusitisha safari yake kwa muda akielekea
Iringa iliasaidi Majeruhi wa ajali ya Roli Kubwa lililokuwa likitokea Dsm
kuelekea Barabara ya Iringa.
Ajali hiyo ambayo ilitokea mbele ya Mh:Mwigulu Nchemba
aliyekuwa nyuma ya Roli hilo kabla ya Kugonga Ukuta na Kuanguka haikuleta
madhara makubwa.
Mh:Mwigulu Nchemba ambaye ni mara kadhaa amekuwa akisaidia
kuokoa majeruhi kwenye ajali anapokutana nazo barabarani,hata kwenye ajali hii
alilazimika kuhakikisha majeruhi wanaokolewa na kukimbizwa Hospitali kabla ya
hatua kubwa zaidi za Hospitali kuendelea,Katika ajali hiyo Mh:Mwigulu Nchemba
alitumia Boksi lake la Msalaba Mwekundu(First Aid Kit) kuhudumia majeruhi hao
iliwasitoke sana Damu.
Wananchi na Madreva waliopata kusimama kwenye ajali
hiyo,Walimpongea sana Mh:Mwigulu Nchemba kwa namna alivyosaidia kuokoa
Watanzania wenzake kwenye ajali hiyo,Wengi walisikika wakiomba Viongozi wengine
waige mifano hii ya Mwigulu ya Kusimama na kuhudumia wahanga wa ajali,Kwa
sababu imekuwa ikitokea Viongozi wanapoona ajali hawasimami kwa madai wanawahi
ratiba za kazi zao.
|
No comments:
Post a Comment