Wakati wajumbe wa Bunge la Katiba wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakiendelea na msimamo wa kususia vikao vinavyotarajiwa kuanza leo mjini Dodoma, mmoja wa wajumbe wake jana aliripoti bungeni na kujiandikisha.
Mjumbe huyo, Clara Mwatuka ambaye pia ni Mbunge wa Viti Maalumu (CUF), alionekana katika Viwanja vya Bunge saa 6:30 mchana akiwa
ameongozana na wabunge kadhaa wa CCM wakiwamo Livingstone Lusinde (Mtera) na Jerome Bwanausi (Lulindi).
ameongozana na wabunge kadhaa wa CCM wakiwamo Livingstone Lusinde (Mtera) na Jerome Bwanausi (Lulindi).
CUF ni moja ya vyama vinavyounda Ukawa, pamoja na Chadema na NCCR Mageuzi na tayari viongozi wakuu wa vyama hivyo, Profesa Ibrahim Lipumba, Freeman Mbowe na James Mbatia wametangaza kwamba wajumbe wote wanaotokana na umoja wao hawatashiriki vikao vya Bunge hilo.
Mwatuka baada ya kujaza fomu maalumu za kujiandikisha, alielekea lango la Magharibi na kuingia kwenye gari la Bwanausi.
Awali, alipoulizwa kwenye Viwanja vya Bunge kuhusu kuwapo kwake Dodoma, alikataa kuzungumza lakini alikiri kujiandikisha bungeni.
No comments:
Post a Comment