Shabiki wa klabu ya Liverpool aliyekuwa mmoja wa mashuhuda
wa mchezo wa hatua ya fainali ya michuano ya Champions Cup uliochezwa nchini
Marekani mapema hii leo, ameacha kibweka nchini humo baada ya
kuvaa flana
ambayo inakebehi kitendo cha utovu wa nidhamu kilichoonyeshwa na aliyekuwa
mshambuliaji wa klabu hiyo Luis Suarez, wakati wa fainali za kombe la dunia za
mwaka huu zilizochezwa nchini Brazil.
Shabiki huyo mwanadada alionekana akiwa amevalia flana yenye
maandishi yaliyosomeka “Suarez Was Here” akimaanisha “Suarez alikuwepo hapa” na
sehemu ya bega lake pameokana na tundu lililonakshiwa sehemu ya memo.
Hata hivyo shabiki huyo hakuonekana kujali sana licha ya
kuvaa flana hiyo ambayo iliwakumbusha mbali mashabiki wenzake ambao alikuwa
amekaanao jukwani wakifuatilia mchezo wa Man Utd dhidi ya Liverpool.
Kama itakumbukwa vyema Luis Suarez kwa sasa anakabiliwa na
kifungo cha kutojihusisha na masuala ya soka kwa muda wa miezi minne, baada ya
kubainika alimng’ata kwa makusudi beki wa timu ya taifa ya Italia Georgio
Chiellini
No comments:
Post a Comment