Pages

Monday, August 18, 2014

MWILI WA KICHANGA WAKUTWA UMEFUKIWA KWENYE GOFU SONGEA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiXLWLU_JBAnflJ4SyaWZlY5UGM4VHl809p3ijPGfRZmaH5JXp2gDUFAuKbUTfky4wbMb3EfBSBBgtHWB8fiZq_kRA7sx_bru5V9NojdNwYS0eNJHehzTebACh1XPKHSOo9XvZchOZ_tTA/s1600/KAMANDA+WA+POLICE+RUVUMA.JPG
Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela
------------------------------- 
Na Nathan Mtega wa demashonews,Songea
Pamoja na kuwepo kwa harakati na utetezi kuhusiana na haki za watoto ikiwemo ya kuishi lakini bado wilayani Songea mkoani Ruvuma kumeendelea kuwepo kwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinavyoambatana na utupaji wa watoto wachanga.


Vitendo hivyo ni pamoja na kitendo kilichotokea jana katika mtaa wa Lizaboni mjini Songea ambapo mwili wa mtoto mchanga anaedaiwa kuwa na umri wa miezi sita ulikutwa ukiwa umefukiwa ndani ya nyumba moja ambayo haikaliwi na mtu katika eneo hilo inayomilikiwa na Olaph Ngalika.

 Akizungumzia tukio hilo balozi wa mtaa huo Juma Kanganya amesema taarifa za kuwepo kwa mwili huo zilitolewa na mafundi waliokuwa wakijenga nyumba hiyo ambaye alisema wanahisi kuwepo kwa kiumbe kilichofukiwa ndani ya nyumba hiyo ambacho kinafanana na binadamu.

 Amesema baada ya kupata taarifa hiyo walitoa taarifa polisi ambao walifika na kufukuwa na kukuta sehemu ya mwili wa kichanga kinachodaiwa kuwa na umri wa miezi sita kitendo ambacho mbali ya kuwasghangaza mashuhuda wa tukio hilo lakini wamelionba jeshi la polisi mkoani Ruvuma kufanya uchunguzi wa kina ili kuweza kuwabaini wahusika wa tukio hilo la kikatili.

Kamanda wa polisi mkoa wa Ruvuma Mihayo Msekhela amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema jeshi hilo linaendelea na uchunguzi ili kubaini wahusika wa kitendo hicho ili hatua za kisheria ziweze kuchukuliwa dhidi yao huku baadhi ya wanaharakati wa haki za watoto wakitoa wito kwa jamii mkoani Ruvuma kutoa ushirikiano kwa vyombo vya dola ili kuweza kudhibiti vitendo hivyo vya ukatili kwa watoto.

Mwisho.

No comments:

Post a Comment