Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Thursday, August 28, 2014

TAARIFA KWA UMMA TOKA MANISPAA YA KINONDONI


Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa katika Mkutano maalumu wa leo Alhamisi tarehe 28/08/2014 pamoja na mambo Mengine, lilimchagua Naibu Meya wa Manispaa na wenyeviti wa kamati mbalmali za kudumu watakao fanyakazi kwa Mwaka huu wa fedha 2014/2015.

Katika uchaguzi wa Naibu Meya, kulikuwa na wagombea wawili ambao ni Ephraim Kinyafu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na Mh. Songoro Hamisi Mnyonge wa Chama cha Mapinduzi ( CCM).
Matokea yaliyotangazwa ni yanaonyesha kuwa , Kura zilizopigwa zilikuwa 41, Kura zilizoharibika 0. Mh.Ephraim Kinyafu amepata kura 13, na Mh. Songoro Hamisi Mnyonge kura 28. Hivyo Mh. Songoro Hamis Mnyonge ameweza kutetea kiti chake cha unabu Meya kwa mara nyingine na Kuwa Naibu Meya wa Kwanza kuongoza Halmashauri kwa nafasi ya unaibu Meya kwa kipindi cha miaka mitano mfululizo kwa kushinda kila mwaka kutetea kiti chake.
Aidha Mkutano huo maalum wa Baraza la Madiwani uliunda kamati Mbalimbali za kudumu za Manispaa kwa Mwaka 2014/2015 na kupitisha ratiba za vikaovya Kamati ya kudumu kwa Mwaka mzima na kuchagua wenyeviti wa Kamati hizo, ambapo Mh. Clement Boko, Diwani wa Mabwepande, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa huduma za Uchumi, Afya na Elimu, Mh. Richard Chengula, Diwani wa Kigogo amechaguliwa tena kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mipangomiji na Mazingira. Kamati nyingine za Kudumu ni Kamati ya Fedha na Uongozi inayoongozwa na Mstahiki Meya, Mh Yusuph juma Mwenda na Kamati ya Kudhibiti ukimwi inayoongozwa na Naibu Meya Mh. Hamis Songoro Mnyonge.
Baraza la Madiwani limeazimia kutoa ushirikiano mkubwa kwa viongozi wote na watendaji wa Manispaa ili kuendeleza mafanikio yaliyofikiwa na kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa Wananchi.
Imetolewa na
ENG. MUSSA NATTY
MKURUGENZI WA MANISPAA

HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI.

No comments:

Post a Comment