Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
chini ya Mstahiki Meya wa Manispaa katika Mkutano maalumu wa leo Alhamisi
tarehe 28/08/2014 pamoja na mambo Mengine, lilimchagua Naibu Meya wa Manispaa
na wenyeviti wa kamati mbalmali za kudumu watakao fanyakazi kwa Mwaka huu wa
fedha 2014/2015.
Katika uchaguzi wa Naibu Meya, kulikuwa na wagombea wawili
ambao ni Ephraim Kinyafu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) na
Mh. Songoro Hamisi Mnyonge wa Chama cha Mapinduzi ( CCM).
Matokea yaliyotangazwa ni yanaonyesha kuwa , Kura
zilizopigwa zilikuwa 41, Kura zilizoharibika 0. Mh.Ephraim Kinyafu amepata kura
13, na Mh. Songoro Hamisi Mnyonge kura 28. Hivyo Mh. Songoro Hamis Mnyonge
ameweza kutetea kiti chake cha unabu Meya kwa mara nyingine na Kuwa Naibu Meya
wa Kwanza kuongoza Halmashauri kwa nafasi ya unaibu Meya kwa kipindi cha miaka
mitano mfululizo kwa kushinda kila mwaka kutetea kiti chake.
Aidha Mkutano huo maalum wa Baraza la Madiwani uliunda
kamati Mbalimbali za kudumu za Manispaa kwa Mwaka 2014/2015 na kupitisha ratiba
za vikaovya Kamati ya kudumu kwa Mwaka mzima na kuchagua wenyeviti wa Kamati
hizo, ambapo Mh. Clement Boko, Diwani wa Mabwepande, amechaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa huduma za Uchumi, Afya na Elimu, Mh. Richard Chengula, Diwani wa
Kigogo amechaguliwa tena kwa mara nyingine kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya
Mipangomiji na Mazingira. Kamati nyingine za Kudumu ni Kamati ya Fedha na
Uongozi inayoongozwa na Mstahiki Meya, Mh Yusuph juma Mwenda na Kamati ya
Kudhibiti ukimwi inayoongozwa na Naibu Meya Mh. Hamis Songoro Mnyonge.
Baraza la Madiwani limeazimia kutoa ushirikiano mkubwa kwa
viongozi wote na watendaji wa Manispaa ili kuendeleza mafanikio yaliyofikiwa na
kuwezesha utoaji wa huduma bora kwa Wananchi.
Imetolewa na
ENG. MUSSA NATTY
MKURUGENZI WA MANISPAA
HALMASHAURI YA MANISPAA YA KINONDONI.
No comments:
Post a Comment