“Mimi nimefanya hivi kwa kupenda kwangu, sijalazimishwa na
mtu. Nimejisikia kufanya hivi kwa sababu nampenda sana Shilole…tukiachana basi
lakini mimi nitabaki nayo hadi nitakapoenda kaburini.” Nuh aliiambia tovuti ya
Times Fm.
Hata hivyo, Shilole alisema kuwa hatajichora kwa kuwa Nuh
kafanya hivyo na kwamba anashukuru kwa uamuzi wake kwa kuwa hakulazimishwa na
ni ishara ya upendo wa kweli tofauti na aliowahi kukutana nao awali.
“Siwezi kusema ntafanya hivyo sijui na nini basi ni mapenzi
tu na mimi siku nikiamua kufanya ntafanya kama ambavyo amefanya yeye. Kiukweli
ana love ya ukweli kabisa tofauti na wanaume ambao nilikuwa nao, watu walikuwa
wanapenda tu wasikie wanatoka na ShiShi kwa kutaka kutafuta kick na lakini Nuh
kama Nuh ana upendo wa peke yake kabisa. Yaani hadi inafikia hatua nasema alikuwa
wapi. Wanasema Mungu akitaka kukupa kitu hakuandikii barua.”
Uamuzi wa Nuh Mziwanda unaendana na uamuzi alioufanya Nick
Cannon na Mariah Carey mwaka 2008 walipojichora tattoo za kudumu kwenye miili
yao baada ya kufunga ndoa. Nick aliandika mgongoni ‘Mariah’, na Mariah
alijichora kipepeo chini ya mgongo na kuandika maandishi madogo ‘Mrs Cannon’.
“Kwangu mimi pete ni maalum na zinavutia, lakini tattoo
zinamaana zaidi kitu chochote. Ni za milele na milele…” Alisema Mariah Carey.
Hivi sasa Mariah na Nick Cannon wametengana na kwa mujibu wa
vyanzo vya uhakika wanasubiri talaka tu.Lakini wamebaki na alama za tattoo
kwenye maisha yao ambazo hazitafutika daima hata watakapokuwa na wapenzi
wengine.Hata hivyo, tattoo inaweza isiwe kitu kama watoto wao mapacha ambapo
pia ni kiunganishi kikubwa katika maisha yao.
Je, Nuh Mziwanda na Shilole wao watafikia hatua ipi? Je,
watadumu kama tattoo ya Nuh Mziwanda au watayeyuka na kuachiana alama za
maandishi
No comments:
Post a Comment