Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Saturday, August 30, 2014

TAZAMA HIZI PICHA ZA SHILOLE NA NUH MZIWANDA JE WALICOPY KWA MARIA CAREY NA NICK CANON?



Mwimbaji wa Bongo Flava, Nuh Mziwanda aliwashitua wengi baada ya kujichora tattoo yenye jina la mpenzi wake ‘Shilole’, tattoo ambayo haifutiki daima. Kitu ambacho kiliwashitua wengi.


“Mimi nimefanya hivi kwa kupenda kwangu, sijalazimishwa na mtu. Nimejisikia kufanya hivi kwa sababu nampenda sana Shilole…tukiachana basi lakini mimi nitabaki nayo hadi nitakapoenda kaburini.” Nuh aliiambia tovuti ya Times Fm.

Hata hivyo, Shilole alisema kuwa hatajichora kwa kuwa Nuh kafanya hivyo na kwamba anashukuru kwa uamuzi wake kwa kuwa hakulazimishwa na ni ishara ya upendo wa kweli tofauti na aliowahi kukutana nao awali.
“Siwezi kusema ntafanya hivyo sijui na nini basi ni mapenzi tu na mimi siku nikiamua kufanya ntafanya kama ambavyo amefanya yeye. Kiukweli ana love ya ukweli kabisa tofauti na wanaume ambao nilikuwa nao, watu walikuwa wanapenda tu wasikie wanatoka na ShiShi kwa kutaka kutafuta kick na lakini Nuh kama Nuh ana upendo wa peke yake kabisa. Yaani hadi inafikia hatua nasema alikuwa wapi. Wanasema Mungu akitaka kukupa kitu hakuandikii barua.”
 Uamuzi wa Nuh Mziwanda unaendana na uamuzi alioufanya Nick Cannon na Mariah Carey mwaka 2008 walipojichora tattoo za kudumu kwenye miili yao baada ya kufunga ndoa. Nick aliandika mgongoni ‘Mariah’, na Mariah alijichora kipepeo chini ya mgongo na kuandika maandishi madogo ‘Mrs Cannon’.
“Kwangu mimi pete ni maalum na zinavutia, lakini tattoo zinamaana zaidi kitu chochote. Ni za milele na milele…” Alisema Mariah Carey.
 Hivi sasa Mariah na Nick Cannon wametengana na kwa mujibu wa vyanzo vya uhakika wanasubiri talaka tu.Lakini wamebaki na alama za tattoo kwenye maisha yao ambazo hazitafutika daima hata watakapokuwa na wapenzi wengine.Hata hivyo, tattoo inaweza isiwe kitu kama watoto wao mapacha ambapo pia ni kiunganishi kikubwa katika maisha yao.

Je, Nuh Mziwanda na Shilole wao watafikia hatua ipi? Je, watadumu kama tattoo ya Nuh Mziwanda au watayeyuka na kuachiana alama za maandishi

No comments:

Post a Comment