Pages

Tuesday, August 19, 2014

TAZAMA PICHA ZA ALBINO WAANDAMANA NA KUZUA TAFRANI POLISI BUGURUNI.

Wakazi wa Dar es Salaam ambao ni walemavu wa ngozi (albino) wakionesha hisia zao nje ya Kituo cha Polisi Buguruni, Dar es Salaam baada ya mtuhumiwa wa kutishia mauaji ya mwenzao aliyefikishwa kituoni hapo jana kudaiwa kuachiwa kwa dhamana jambo ambalo walilipinga. (Picha na Fadhili Akida).

Wakazi wa Dar es Salaam ambao ni walemavu wa ngozi (albino) wakionesha hisia zao nje ya Kituo cha Polisi Buguruni, Dar es Salaam baada ya mtuhumiwa wa kutishia mauaji ya mwenzao aliyefikishwa kituoni hapo jana kudaiwa kuachiwa kwa dhamana jambo ambalo walilipinga.Watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), jana walizua tafrani Kituo cha Polisi Buguruni, wakipinga dhamana kwa mshtakiwa, Ombeni Swai (34), mkazi wa Tabata Matumbi anayekabiliwa na kesi ya kutoa vitisho vya kumuua mwenzao.



Tafrani hiyo ilianzia katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni baada ya mshtakiwa huyo kusomewa mashtaka na Karani wa Mahakama, Edwin Wandanda na kisha Hakimu Mfawidhi, Benjamin Mwakasonda aliyekuwa akiisikiliza kusema dhamana ya mshtakiwa iko wazi.
Polisi wa Kituo cha Bungurini wakiwa na silaha zinazodaiwa kutumiwa kuwatawanya watu wenye ulemavu wa ngozi kitioni hapo wakati wakizuia gari ilikuwa imebeba mtu anayetuhumiwa kumuua Albino baada ya kufunguliwa mashitika katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni.
Ingawa mshtakiwa alishindwa kutimiza masharti ya dhamana, albino waliokuwapo mahakamani hapo hawakufurahishwa na kitendo cha kuwapo kwa nafasi ya dhamana kwa mshtakiwa wakidai kwamba ameshatoa vitisho vya mauaji dhidi yao.
Baada ya kulalamika mahakamani hapo waliandamana hadi kituoni hapo ambako mshtakiwa alikuwa amepelekwa hali iliyosababisha polisi kituoni hapo kutumia risasi za baridi kuwatawanya na kusababisha taharuki kwa wafanyabiashara na wakazi wa eneo hilo.
Mwandishi wetu alishuhudia baadhi ya watu wakiwa wamesimama, wengine wakikimbia ovyo huku polisi wakiwa silaha.
Kamanda wa Mkoa wa Polisi Ilala, Mariam Nzuki alisema vurugu hizo ziliongezeka baada ya kundi la vijana wa sokoni kuungana nao.
Alisema baada ya polisi kuona hivyo, walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya na kumpeleka mtuhumiwa katika Mahabusu ya Segerea.

Hati ya mashtaka
Mshtakiwa anadaiwa kuwa Agosti 16, mwaka huu maeneo ya Buguruni kwa Mkanda alitishia kuua kwa maneno watu wenye ulemavu wa ngozi katika maeneo hayo.
Hati hiyo inadai kuwa mshtakiwa alimtishia kwa maneno mlalamikaji, Mwinyiusi Issa kuwa atamuua kama anavyoua albino.
Mengi ajitolea Wakati hayo yakitokea, Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi amejitolea kuwasomesha watoto wawili wa albino Suzan Mungi, aliyekatwa kiganja cha mkono na watu wasiojulikana wilayani Igunga mkoani Tabora.
Akizungumza jana, Mengi alisema amesikitishwa na tukio hilo ambalo mume wa Suzan, Mapambo Mashili aliuawa wakati akijaribu kumtetea ili asifanyiwe ukatili huo.
“Sina mamlaka ya kuwaadhibiti wahalifu hawa lakini naahidi kutoa Sh10 milioni kwa mtu atakayewezesha kukamatwa kwao, Serikali inapaswa kuwashughulikia wahusika wote yaani wanaofanya ukatili huo, wanaohitaji viungo hivyo na waganga wa kienyeji,” alisema.

No comments:

Post a Comment