Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Monday, August 4, 2014

WAKE WA VIONGOZI WAMTEMBELEA MAMA MARIA NYERERE NYUMBANI KWAKE MSASANI


Mke wa Waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda (kulia) ambaye ni mlezi wa kikundi cha Wake waViongozi (NEW MELLENIUMWOMEN GROUP) akimsikiliza kwa makini Mama Maria Nyerere wakati walipo mtembelea nyumbani kwake kwa ajili yakumjulia hali pamoja na kumpatia zawadi mbalimbali kutokana na mchango wake mkubwa aliokuwa anampa Baba wa Taifa ambao ulisaidia kuleta amani utulivu na maendeleo ndani ya nchi na nje ya Tanzania.
Mama Maria Nyerere na MamaTunu Pinda wakiangali picha zao walizo pigwa na Mama Othmani kwenye simu ya kiganjani wakati kikundi cha wake wa viongozi (NEW MELLENIUMWOMEN GROUP) walipo mtembelea Mama Nyerere nyumbani kwake Msasani kumjulia hali. 

Kikundi cha wake wa viongozi wakiwa katika picha ya pamoja na Mama Maria Nyerere walioketi (katikati) Mama Tunu Pinda Mama (wa pili kushoto walioketi) Mama Regina Lowasa (kushoto) Mama Sophia Kawawa (wa pili kulia walioketi) akifuatiwa na Mama Sumaye.Picha na Chris Mfinanga.

No comments:

Post a Comment