Kijana aliyekatwa na sime kichwani.
Timbwili lenye ujazo
mkubwa limeibuka baa ambapo jamaa mmoja muokota chupa za maji ambaye jina lake
halikupatikana, anadaiwa kukatwa sime kichwani na mwenye gari baada ya kukutwa
amekaa karibu na gari hilo.
Kwa mujibu wa shuhuda wetu, tukio hilo la kuumiza lilijiri
wikiendi iliyopita mishale ya asubuhi kwenye baa mpya iitwayo Kangaroo iliyopo
eneo la Afrika Sana jijini Dar.Ilielezwa kwamba kijana huyo alikuwa amekaa
pembeni ya gari hilo huku akisoma Gazeti Pendwa la Amani ambalo ni ndugu na
hili, mara ghafla alikuja mtu akitokea ndani ya baa kisha akaingia kwenye gari
lake aina ya Toyota Noah akatoka na sime na kuanza kumshambulia jamaa huyo
kichwani.

Polisi akiingia eneo la tukio kutuliza ugomvi uliojitokeza.
“Mimi siyo mwizi,
nilikuwa nimepumzika baada ya kuzunguka sana, nikaamua kutulia na kusoma
gazeti, nimeonewa mimi ni muokota chupa za maji tu,” alisema kijana huyo kwa
uchungu huku akitoa tafsiri ya namna wenye nazo wanavyowanyanyasa maskini
Wanawake wakishudia mkasa huo.
Baada ya kujielezea,
watu waliamua kumfuatilia mwenye gari na kuanza kumpiga wakitaka awaambie
sababu za kumkata kijana huyo.Hali ilipokuwa tete, uongozi wa baa hiyo ulitoa
taarifa kwenye Kituo cha Polisi cha Kijitonyama a.k.a Mabatini, Dar ambapo
askari walitinga katika eneo hilo ndani ya dakika sifuri wakiwa tayari kwa
lolote.
aia walikuwa eneo la tukio.
Askari hao waliokoa
jahazi kwa kuwatuliza raia hao na kuwachukua wahusika wote na kuondoka nao kwa
ajili ya kutoa maelezo kituoni ili sheria ichukue mkondo wake
No comments:
Post a Comment