YULE mtoto wa umri wa
mwaka mmoja na miezi miwili, Regina Geofrey aliyeuawa kikatili kwa
kunyongwa
kisha kuzikwa na baba yake mzazi, Geofrey Kilangwa ‘Simbaiwe’ (27) kwa kuwa
alizaliwa akiwa ametanguliza makalio yake, amezidi kuibua maswali.Baadhi ya
wakazi wa Katavi waliozungumza na gazeti hili juzi, walihoji uhalali wa baba
kumjadili mtoto katika kuzaliwa kwa sababu ya kutanguliza kiungo fulani.Wengine
walitaka kujua ni kwa nini kama kumuua mtoto wake, mzazi huyo alisubiri kwa
mwaka mmoja na miezi miwili? Mtuhumiwa ambaye pia ni mganga wa kienyeji
anayeishi Kitongoji cha Mwikang’ombe, Kijiji cha Katuma wilayani Mpanda,
alitenda unyama huo kwa madai kuwa mtoto
huyo alizaliwa akiwa ametanguliza makalio, hivyo ni nuksi kubwa katika shughuli
zake za uganga wa kienyeji, madai yaliyopingwa na watu mbalimbali, zikiwemo
taasisi za kutetea haki za binadamu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, akizungumza na waandishi wa habari mjini
hapa, alidai mzazi huyo alitenda uhalifu huo Agosti 20, mwaka huu
ambapo alikamatwa na Jeshi la Polisi, Agosti 26.
Ilidaiwa siku hiyo ya
tukio, mtuhumiwa huyo baada ya kumnyonga hadi kufa binti yake,
alimzika kwa siri katika kibanda chake anachofanyia shughuli za uganga.
Kamanda Kidavashari alisema mtoto Regina alikuwa
anasumbuliwa na ugonjwa ambao haukufahamika
kwa zaidi ya mwezi mmoja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari.
“Ndipo baba mzazi
wa binti huyo alipomchukua marehemu na kwenda kumuuguza kwa
siri pasipo mama yake mzazi kufahamu
kwani alimdanganya kuwa mtoto wao amepelekwa
kutibiwa na babu yake mkoani Mwanza,” alisema Kidavashari.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, wakazi wa kitongoji hicho wakiongozwa na mwenyekiti
wao, walimtilia shaka mtuhumiwa kutokana na tetesi zilizosambaa kwamba, Regina
aliuawa na baba yake mzazi na kuzikwa kwa siri.
Mwenyekiti huyo na wakazi wa eneo hilo walifika nyumbani kwa
mtuhumiwa na kuhoji alipo binti yake, aliposhindwa kujibu wakasema wampekue
ambapo alipinga vikali lakini
alipopekuliwa kibandani kwake walibaini kuwepo kwa tuta dogo
lililokuwa limechimbwa siku za karibuni.
Wakazi hao walifukua tuta hilo na kukuta kichwa cha mtoto Regina na ndipo
wakalitaarifu jeshi la polisi.
Mama wa marehemu,
Maria Exavery (22) alisema hakupewa taarifa kwamba binti yake amekufa.
“Mimi nilikuwa nafahamu Regina yuko kwa babu yake Mwanza
akitibiwa,” alisema huku akimwaga machozi.
Naye Regina Kaboni (40), mkazi wa Isamilo Mwanza ambaye alikuwa akitibiwa na mtuhumiwa, anadai kuwa alishirikishwa katika maziko ya
binti huyo baada ya kufa.“Hata hivyo, nilishtushwa sana kwa kitendo cha mtuhumiwa
kumzika mwanaye bila mkewe, nilipomuuliza akadai mila za kwao
mtoto aliyezaliwa kwa kutanguliza
makalio, mama mzazi wa mtoto ni mwiko
kushirikishwa katika maziko.
Kwa mujibu wa Kidavashari watu wanne, wakiwemo wazazi
wa marehemu wanashikiliwa na
Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi ambapo watafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi kukamilika.
Wengine
wanaoshikiliwa na jeshi hilo ni Regina
Kaboni na Msolwa Jacob (29), mkazi wa Kitongoji cha Mwikang’ombe.
No comments:
Post a Comment