Pages

Thursday, September 4, 2014

MIROSLAV KLOSE, PHILIPP LAHM NA MERTESACKER WAPEWA TUZO ZA HESHIMA

Per Mertesacker, Miroslav Klose na Philipp Lahm baada ya kukabidhiwa tuzo zao Esprit Arena
WAKONGWE Miroslav Klose, Philipp Lahm na Per Mertesacker wamepewa tuzo za heshima usiku huu kabla ya mchezo wa kirafiki kati ya Ujerumani na 


Argentina Uwanja wa Esprit Arena.Watatu hao waliichezea Ujerumani katika fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2014 dhidi ya Argentina kabla ya kuamua kustaafu soka ya kimataifa.
Klose, ambaye ni mfungaji bora wa kihistoria wa Ujerumani kwa mabao yake 71, ametungika daluga baada ya kuwa mfungaji wa mabao mengi zaidi katika historia ya Kombe la Dunia.
MCHANGO WAO KATIKA TIMU YA TAIFA UJERUMANI...
Miroslav Klose (Lazio) - Mechi 137, mabao 71
Philipp Lahm (Bayern Munich) - Mechi 113, mabao 5

Per Mertesacker (Arsenal) - Mechi 104, mabao 4

No comments:

Post a Comment