Msemaji wa Rais alikana kuwa gari hilo lilikuwa limeibwa
Maafisa wakuu kutoka shirika la polisi wa kimataifa,
Interpol amethibitisha kuwa gari la ulinzi wa rais Uhuru Kenyatta lililoibwa
mjini Nairobi wiki jana limepatikana nchini Uganda.
Kwa sasa gari hilo limepelekwa mjini Kampala.
Gari hilo aina ya BMW liliibwa siku ya Jumatano usiku mjini
Nairobi. Watu watatu wamekamatwa kuhusiana na wizi huo.
Mkurugenzi wa polisi wa kimataifa Interpol nchini Uganda
Assab Kasingye aliambia BBC kuwa gari hilo litarudishwa Nairobi.
Gari hilo liliibwa na watu waliokuwa wamejihami Jumatano
wiki jana.
Hata hivyo msemaji wa serikali Manoah Esipisu alikanusha
habari hizo akisema kuwa gari lililoibwa halikuwa na ulinzi wa Rais Kenyatta
bali lilikuwa gari kuu kuu la polisi.
Lakini lilikuwa linaendeshwa na afisa wa polisi aliyeripoti
kuwa gari hilo ni mmoja ya magari ya ulinzi wa Rais.Afisa huyo wa polisi pia
alisemekana kuwa mmoja wa maafisa wa polisi wa ulinzi wa Rais.
Tukio la wizi wa gari hilo, lilisababisha taharuki miongoni
mwa maafisa wa ulinzi kwa sababu magari ya ulinzi wa Rais yenyewe yanapaswa
kuwa na ulinzi mkali.
Takwimu za polisi zinaonyesha kuwa visa vitatu vya wizi wa
magari huripotiwa mjini Nairobi kila siku.
Hiki ni kisa kimoja kati ya vingi vya wizi wa magari ambapo
mtu yeyote anaweza kuathirika.
No comments:
Post a Comment