Wizara ya ulinzi ya Marekani inasema kuwa jeshi la nchi hiyo
limefanya mashambulizi dhidi ya kundi la wanamgambo wa kiislamu la , Al Shabaab
nchini Somalia.
Msemaji wa Pentagon Rear Admiral John Kirby amesema kuwa
wanatathmini matokeo ya operesheni hiyo kabla ya kutoa taarifa zaidi .
Al Shabaab kwa sasa wanaendesha kampeni dhidi ya
serikali ya
Somalia na vikosi vya kimataifa vinavyoiunga mkono.
Wanajeshi wa Muungano wa Afrika
Afisa mkuu wa Marekani amesema kuwa maafisa wakuu wa Al
Shabaab ndio waliolengwa kwenye mashambulizi hayo.
Kundi hilo lenya uhusiano na al-Qaeda lilitimuliwa kutoka
Mogadishu mwaka 2011 mji ambao kwa sasa unadhibitiwa na wanajeshi wa Muungano
wa Afrika.
Hata hivyo kundi hilo bado linadhibiti maeneo ya Kusini ya
nchi hiyo
Mkazi mmoja alinukuliwa akisema alishuhudia moshi mkubwa
ukifuka
Tungali tunadadisi hali na matokeo ya shambulizi na baadaye
tutaweza kutoa maelezo,'' alisema msemaji wa mkuu wa Pentagon
Wakazi wa kijiji cha Hawai umbali wa kilomita 240 Kusini mwa
Mogadishu, wanasema kuwa walisikia milipuko na kisha kuona moshi mkubwa
ukifuka.
Mkazi mmoja aliambia BBC kwamba aliona mabaki ya gari moja
liliokuwa limelipuliwa ingawa hakuona miili yoyote.
No comments:
Post a Comment