Shirika la afya duniani likishirikiana na wizara ya afya
katika Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo imesema kuwa mlipuko wa ugonjwa wa
Ebola nchini humo umewaua watu 31.
Ugonjwa huo ulipatikana mapema mwezi uliopita katika nchi
hiyo karibu na mji wa Boende takriban
kilomita mia nane kazkazini mwa mji mkuu
wa Kinshasa.
Maafisa wanasema kuwa eneo hilo limewekwa karantini na zaidi
ya watu 50 wanapokea matibabu baada ya kuambukizwa maradhi hayo.
Takriban watu 200 wanachunguzwa. Wizara ya afya mjini
Kinshasa imesisitiza kuwa mlipuko wa homa hiyo haihusishwa na mlipuko wa Ebola
uliotikisa kanda ya Afrika Magharibi ambako zaidi ya watu 1500 wamefariki.
No comments:
Post a Comment