THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE
OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425
|
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,
Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia Salamu za Rambirambi Mkuu wa
Mkoa wa Mbeya, Mheshimiwa Abbas Kandoro kuomboleza vifo vya watu 10
vilivyotokea Mbalizi, Mkoani Mbeya tarehe 29 Agosti, 2014 baada ya basi dogo la
abiria aina ya Toyota Hiace maarufu kama Daladala Na. T 237 BFB kugongana na
lori aina ya Tata Na. T 158 CSV. Katika
ajali hiyo, watu saba wengine walijeruhiwa na kukimbizwa hospitali kwa
matibabu.
“Nimesikitishwa
na kuhuzunishwa mno na taarifa za vifo vya watu 10 na wengine saba kujeruhiwa
katika ajali hii iliyotokea siku chache baada ya ajali nyingine kutokea Mkoani
Tabora iliyoua watu 19 na wengine 81 kujeruhiwa”, amesema
Rais katika salamu zake.
Rais
Kikwete amesema mfululizo wa ajali hizi unaonyesha dhahiri kuendelea kuwepo kwa
tatizo la ukosefu wa umakini miongoni mwa madereva, hivyo jitihada zaidi zinatakiwa
kufanywa kusimamia kikamilifu Sheria ya Usalama Barabarani na kufuatiliwa kwa
karibu kwa mienendo ya wanaoendesha vyombo vya moto, ili ajali hizi ziweze kupunguzwa
na hata kudhibitiwa kabisa katika barabara zetu.
“Naomba
upokee salamu zangu za rambirambi kutoka dhati ya moyo wangu kutokana na ajali
hiyo, na kupitia kwako naomba unifikishie salamu zangu za pole kwa wafiwa wote
kwa kupotelewa ghafla na wapendwa wao”Ameongeza.
Rais
Kikwete amesema anatambua machungu waliyo nayo wanafamilia, ndugu na jamaa wa
watu waliopoteza maisha yao kwenye ajali hiyo, lakini anawaomba wote wawe wavumilivu
na wenye subira wakati huu wanapoomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao.
“Ninawaombea
kwa Mola majeruhi wote wa ajali hiyo waweze kupona haraka na kurejea katika
hali zao za kawaida ili waweze kuungana
tena na familia, ndugu na jamaa zao”,
amemalizia
kusema Rais Kikwete katika salamu zake.
Imetolewa na;
Kurugenzi ya Mawasiliano ya
Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam .
31 Agosti,2014
No comments:
Post a Comment