Pages

Monday, September 15, 2014

KATIBU MKUU WA CCM,NDUGU KINANA AANZA ZIARA YAKE MIKOA YA PWANI,TANGA NA IRINGA


1 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kata ya Kimanzichana leo wakati alipoanza Ziara yake ya mikoa ya Pwani ,Tanga na Iringa Ikiwa ni kuimarisha Chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 huku akihimiza wananchi kushiriki katika shughuli za kujiletea maendeleo katika maeneo yao, Katibu Mkuu Abdulrahman Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi na amefanya shughuli mbalimbali katika ziara hiyo.



2 
Mbunge wa jimbo la Mkuruanga na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Adama Malima akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mkuranga wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo  3 
Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi akizungumza na wananchi wa kata ya Kimanzichana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapo 4 
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Mercy Silla akwahutubia wananchi wa kata ya Kimanzichana kwenye mkutano wa hadhara5 
Baadhi ya wananchi wakipunga mikono kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo pichani wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kimanzichana. 6 
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano mjini Kimanzichana, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkuranga.

No comments:

Post a Comment