Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwahutubia wananchi wa Kata ya
Kimanzichana leo wakati alipoanza Ziara yake ya mikoa ya Pwani ,Tanga na
Iringa Ikiwa ni kuimarisha Chama na kukagua utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi ya Mwaka 2010 huku akihimiza wananchi kushiriki katika shughuli
za kujiletea maendeleo katika maeneo yao, Katibu Mkuu Abdulrahman
Kinana anaongozana na Nape Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi
na amefanya shughuli mbalimbali katika ziara hiyo.
Mbunge
wa jimbo la Mkuruanga na Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi Mh. Adama
Malima akizungumza na wananchi katika kijiji cha Mkuranga wakati wa
mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata hiyo
Nape
Nnauye Katibu wa NEC Siasa Itikadi na Uenezi akizungumza na wananchi wa
kata ya Kimanzichana wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika mjini
hapo
Mkuu wa Wilaya ya Mkuranga Mh. Mercy Silla akwahutubia wananchi wa kata ya Kimanzichana kwenye mkutano wa hadhara
Baadhi ya wananchi
wakipunga mikono kwa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana hayupo
pichani wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika kata ya Kimanzichana.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiwapungia
mkono wananchi mara baada ya kuwasili katika eneo la mkutano mjini
Kimanzichana, kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mkuranga.
No comments:
Post a Comment