Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Sunday, September 7, 2014

NEYMAR NA JUAN WASAMEHEHANA,, WAKUMBATIANA

Apology accepted: Juan Zuniga is embraced by Brazil captain Neymar before the friendly match


Msamaha umekubalika: Juan Zuniga alikumbatiwa na nahodha wa Brazil, Neymar kabla ya mechi ya kirafiki kuanza.
NYOTA wa Brazil, Neymar, ameonekana kukubali msamaha wa Mcolombia, Juan Zuniga aliyemvunja mfupa wa uti wa mgongo na kumaliza safari yake ya kucheza fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu katika ardhi ya nyumbani.

 
Neymar aliyeiongoza Brazil kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa nahodha na kocha wa timu ya Taifa, Dunga, alimkumbatia Zuniga kabla ya kuanza mchezo ambao wazee wa Samba walishinda 1-0 katika uwanja wa Sun Life mjini Miami.
Mshambuliaji huyo wa Barcelona alikosa mechi zote zilizosalia za kombe la dunia katika ardhi yake kufuatia kugongana na beki huyo wa Napoli, Zuniga wakati wa mechi ya robo fainali.
Show of affection: Neymar and Zuniga shared a hug at the Sun Life Stadium in Florida, Miami
Akionesha mapenzi: Neymar na Zuniga walikumbatiana katika uwanja wa  Sun Life uliopo Florida, Miami

No comments:

Post a Comment