Msamaha umekubalika: Juan Zuniga alikumbatiwa na nahodha wa Brazil, Neymar kabla ya mechi ya kirafiki kuanza.
NYOTA wa Brazil, Neymar, ameonekana kukubali msamaha wa Mcolombia, Juan Zuniga aliyemvunja mfupa wa uti wa mgongo na kumaliza safari yake ya kucheza fainali za kombe la dunia majira ya kiangazi mwaka huu katika ardhi ya nyumbani.
Neymar aliyeiongoza Brazil kwa mara ya kwanza tangu achaguliwe kuwa nahodha na kocha wa timu ya Taifa, Dunga, alimkumbatia Zuniga kabla ya kuanza mchezo ambao wazee wa Samba walishinda 1-0 katika uwanja wa Sun Life mjini Miami.
Akionesha mapenzi: Neymar na Zuniga walikumbatiana katika uwanja wa Sun Life uliopo Florida, Miami
No comments:
Post a Comment