Social Icons

IMETOSHA

IMETOSHA

Wednesday, September 10, 2014

Tahadhari kuhusu gesi za sumu Angani

Mkuu wa shirika la utabiri wa hali ya anga la Umoja wa Mataifa Michel Jarraud, ametoa tahadharti kuwa dunia nzima inapaswa kushughulikia mabadiliko ya hali ya anga haraka iwezekanavyo la sivyo muda unakwisha.

Takwimu mpya kutoka kwa shirika hilo, 
 
zinaonyesha kuwa viwango vipya vya gesi yenye sumu ya Carbon katika anga ya dunia viko juu zaidi.

Pia shirika hilo linasema kuwa kiwango cha gesi ya sumu ya Carbon Dioxide kinaendelea kuongezeka kwa kasi kuliko hali ilivyokuwa miaka mitatu iliyopita.

Shrika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO, linasema kuwa viwango vya gesi chafu viliongezeka kwa kasi zaidi tangu mwaka 1984.

Bwana Michel Jarraud alisema kuwa hapana shaka kwamba mabadiliko ya hali ya anga yanashuhudiwa na kwamba hali inaendelea kuwa mbaya zaidi.

Umoja wa mataifa unasema kuwa kuongezeka kwa gesi hizo kunasababisha mabadilko mabaya ya hali ya hewa hali ambayo inahitaji kuwe kauli moja ya mkataba wa dunia nzima kuweza kukabiliana na hali hiyo.

No comments:

Post a Comment