Mkuu wa shirika la utabiri wa hali ya anga la Umoja wa
Mataifa Michel Jarraud, ametoa tahadharti kuwa dunia nzima inapaswa
kushughulikia mabadiliko ya hali ya anga haraka iwezekanavyo la sivyo muda
unakwisha.
Takwimu mpya kutoka kwa shirika hilo,
zinaonyesha kuwa
viwango vipya vya gesi yenye sumu ya Carbon katika anga ya dunia viko juu
zaidi.
Pia shirika hilo linasema kuwa kiwango cha gesi ya sumu ya
Carbon Dioxide kinaendelea kuongezeka kwa kasi kuliko hali ilivyokuwa miaka
mitatu iliyopita.
Shrika la utabiri wa hali ya hewa duniani WMO, linasema kuwa
viwango vya gesi chafu viliongezeka kwa kasi zaidi tangu mwaka 1984.
Bwana Michel Jarraud alisema kuwa hapana shaka kwamba
mabadiliko ya hali ya anga yanashuhudiwa na kwamba hali inaendelea kuwa mbaya
zaidi.
Umoja wa mataifa unasema kuwa kuongezeka kwa gesi hizo
kunasababisha mabadilko mabaya ya hali ya hewa hali ambayo inahitaji kuwe kauli
moja ya mkataba wa dunia nzima kuweza kukabiliana na hali hiyo.
No comments:
Post a Comment